Tunda la Topetope. |
FAIDA ZA TOPETOPE
Tope tope ni moja ya
tunda ambalo si rahisi sana kulikuta kwenye majokofu ya watu au kwenye orodha
ya matunda mara baada ya kula.
Pamoja na kwamba
tope tope linaladha nzuri na linafaida zake ndani ya mwili, lakini wengi
hawalitumii sana hivyo leo nimeona nikupatie hizi faida zake kadhaa huenda
zitakufanya uanze kulitumia tunda hili
Miongoni mwa faida
za tunda hili ni pamoja na hizi zifuatazo:-
Tope tope
limesheheni vitamin C imbayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na hivyo
kumfanya mtumiaji kuepuka kusongwa na magonjwa mara kwa mara.
Pia tope tope lina
kiasi cha vitami A ambayo hulifanya tunda hilo kuingia kwenye orodha ya matunda
yenye uwezo wa kuboresha na kulinda afya ya ngozi na nywele.
Aidha, tope tope pia
limesheheni madini ya 'potassium', ambayo nayo husaidia miili yetu kuondokana
na tatizo la maumivu ya hapa na pale ya mifupa.
Kwa wale wenye shida
ya maumivu ya mifupa hasa sehemu za maungio 'joint' wanapotumia tunda hili mara
kwa mara huweza kuwa msaada kwao katika kuondokana na tatizo hilo kutokana na
kuwa na madini ya 'magnesium' ndani yake.
Tunda hili pia lina
nyuzinyuzi 'fiber' za kutosha na hivyo kusaidia kurekebisha mfumo wa mmeng'enyo
wa chakula tumboni na kuepuka tatizo la ukosefu wa choo.
Source: dkmandai.com
No comments:
Post a Comment